Image

Watafiti wa magonjwa wanadai kuwa msongo mkali wa mawazo wakati wa ujauzito unaweza kusababisha hitilafu katika uumbaji wa mtoto na hatimaye mtoto kuzaliwa akiwa mlemavu.


Ripoti ya watafiti hao inazidi kuthibitisha matokeo ya tafiti zilizopita kuwa mama mwenye msongo wa mawazo wakati wa ujauzito kutokana na mambo kama kufukuzwa au kuachishwa kazi, kutengana na mwenza wake au kufiwa ana hatari ya kuzaa mtoto mwenye ulemavu kama vile midomo sungura (cleft lip na cleft palate) au matatizo kwenye uti wa mgongo (spina bifida).

Jopo la watafiti wa kidenmark likiongozwa na Dr Dorthe Hansen walifanya uchunguzi ili kuthibiitisha ukweli na uhakika wa  dhana hii. 

Wakitumia rikodi za taarifa za kitabibu za kipindi cha miaka 12 kutoka 1980 mpaka 1992 kutoka masjala ya Taifa ya kitabibu,  watafiti hao waliweza kuwatambua wajawazito wote waliokumbwa na matatizo makubwa ya kimaisha wakati wa ujauzito na hata miezi 16 kabla ya kupata ujauzito. Matatizo makubwa ya kimaisha yaliyochunguzwa yalikuwa kukumbwa na msiba wa ndugu au jamaa wa karibu, ndugu au jamaa wa karibu kulazwa hospitali kwa mara ya kwanza baada ya kugundulika kuwa na kansa ya aina yeyote au ndugu au jamaa wa karibu kupatwa na ugonjwa wa mshtuko wa moyo. Mambo haya yalichunguzwa kwa kigezo kuwa, mjamzito yeyote aliyewahi kukumbana nayo ana hatari kubwa ya kuwa katika msongo wa mawazo bila kujali tabia yake, kama ana watu wa kumfariji au uwezo wake wa kukabiliana nayo.

Jopo hilo lilichunguza maendeleo ya mimba kwa wajawazito 3,560 ambao walikumbana na matukio hayo kwa kulinganisha na  wajawazito wengine 20,299 ambao hawakukumbana na hali yeyote ambayo ingewasababishia kupata msongo wa mawazo wakati waujauzito.


Matokeo ya uchunguzi wao yalionesha kuwa ulemavu na hitilafu za viungo kwa watoto waliozaliwa ulikuwa mara mbili miongoni mwa  kundi la wajawazito waliokumbwa na msongo mkali wa mawazo ikilinganishwa na kundi la kinamama ambao hawakuwa na hali hiyo. 

Kadhalika ilionekana kuwa wanawake waliowahi kukumbwa na hali kama hiyo katika ujauzito mbili mfululizo za nyuma walikuwa katika hatari kubwa zaidi ya kuzaa watoto wenye ulemavu wa viungo tofauti na wale waliowahi kupatwa na hali hiyo mara moja tu au wale ambao hawakupatwa kabisa.

Ilionekana pia kuwa tukio lililoongeza uwezekano wa mtoto kuzaliwa akiwa na ulemavu wa viungo ilikuwa ni iwapo mjamzito atafiwa na mtoto wake mwingine mkubwa wakati akiwa katika miezi mitatu ya mwanzo wa ujauzito wake huu wa sasa. Hatari ya kuzaa mtoto mlemavu iliongezeka iwapo kifo cha mtoto huyo mkubwa kingetokea bila kutarajiwa kwa mfano kwa ajali.

Wanawake wajawazito wanaopenda kulala chali wapo kwenye hatari ya kuzaa mtoto mfu(stillbirth),kulingana na wanasayansi. Katika utafiti uliofanyika nchini Ghana, wanawake wajawazito ambao walipenda kulala chali wakati wa ujauzito walikuwa kwenye hatari mara tano zaidi ya kuzaa watoto wenye uzito mdogo na kwa wanawake wengine walizaa watoto wafu.

Utafiti huu ulifanyika nchini Ghana kutokana na kuwa kati ya watoto 1000 wanaozaliwa 20 hadi 50 kati yao huwa ni watoto wafu. Hata hivyo, utafiti mpya uliofanyika nchini New Zealand pia umehusisha kulala chali kwa mwanamke mjamzito na idadi kubwa ya watoto wafu wanaozaliwa katika nchi zenye raia wenye kipato kikubwa.

Mkuu wa utafiti huu,Louise O'Brien kutoka chuo kikuu cha Michigan, nchini Marekani amesema kama kutokulala chali wakati wa ujauzito hupunguza uwezekano wa kuzaa mtoto mfu basi ni vizuri kuhamasisha kina mama wajawazito kutolala chali kwani hii ni njia rahisi na isiyokuwa na gharama yoyote ile. Tabia hii ya kulala chali wakati wa ujauzito inaweza kuepukika kwa kuwashauri kina mama wajawazito madhara yanayopatikana kwa kulala chali.

Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha ya kwamba zaidi ya robo ya idadi ya watoto wanaozaliwa wafu inaweza kuepukika kwa kubadilisha staili ya kulala tu kwa wanawake wajawazito.

Ndiyo, kuna uwezekano wa kupata ujauzito mara baada ya kujifungua kabla haujapata mzunguko mwingine wa hedhi. Hii ni kwa sababu, yai la mwanamke huwa linapevuka wiki mbili kabla ya kupa hedhi, yaani siku ya kumi na nne kabla ya tarehe ya kwanza ya kupata hedhi, kwa maana hiyo yai linaweza kupevuka na kuweza kuwa kwenye hatari ya kupata ujauzito bila wewe kutambua. Kwa sababu, kupata kwa hedhi ni matokeo ya yai kutopevushwa.

Kimsingi, ni ngumu kwa mama mjamzito kupata mimba mara tu baada ya kujifungua, hasa kama unanyonyesha. Hii ni kwa sababu, kuna vichocheo au homoni ambazo hutolewa kipindi cha kunyonyesha ambayo huzuia yai kupevuka kwa yai na kusababisha kukosa hedhi kwa miezi kadhaa, kitaalamu lactational Amenorrhea. Kukosa huku hedhi hakukukingi kwa asilimia mia moja kupata ujauzito ndio maana ukijifungua kwenye vituo vya afya au hospitali huwa unashauriwa kuhusu njia bora za uzazi wa mpango pale utakapokuwa tayari kuanza tena kufanya tendo la ndoa.

Wakina mama wengi huwa wanapenda kusubiri kupewa ruhusa na daktari wake wakati wanapoenda kliniki baada ya kujifungua, ingawa wapo ambao huwa wanajisikia wako tayari pale tu damu inapokata au nyuzi na michubukuko ya kupindi cha kujifungua vinapopona.

Kama unanyonyesha na kutumia maziwa ya kopo, hedhi inaweza kurudi baada ya wiki sita mpaka kumi baada ya mtoto kuzaliwa. Kama ni kunyonyesha peke yake inaweza kuchukua kipindi kirefu Zaidi yaani miezi kadhaa, ingawa hamna jibu la moja kwa moja kuhusu  ni lini au ni kipindi kipi unaweza kupata hedhi.

Ni vyema kupata ushauri wa daktarin hata kama ni siku za awali baada ya kujifungua, ili kuweza kupanga mapema na kuamua.

Je naweza kutumia vidonge vya uzazi wa mpango wakati nanyonyesha?

Katika miezi sita ya mwanzo huwa haishauriwi kutumia vidonge vya uzazi wa mpango vyenye mchanganyiko wa homoni au vichocheo kwa maana huweza kupunguza kiasi cha maziwa ambacho hutolewa. Ingawa kutumia kidonge chenye kichocheo aina moja kitaalamu Progesterone only pill huwa ni salama kabisa.

Aina nyingine za uzazi wa mpango ambazo hazishauriwi kwenye kipindicha miezi sita ya mwanzo ambazo pia zina mchanganyiko wa homoni au vichocheo ni zile za kubandika na pete ya uke.

Kipindi unanyonyesha ni vyema kujielimisha na kujifunza njia za uzazi wa mpango

Je wakati gani salama kupata tena ujauzito baada ya kujifungua?

Kama unampngo wa kuongeza mwanafamilia ni vyema kujua kutokana na tafiti mbali mbali angalau baada ya mwaka mmoja mpaka miezi 18 kabla ya kushika ujauzito tena. Tafiti zinaonyesha kuwa kujifungua kabla ya kipindi hiki inaweza kupelekea kujifingua kabla ya wakati (njiti) na kusababisha matatizo ya kiafya kwa mtoto.

Kujipa nafasi kabla ya kupata ujauzito mwingine huupa mwili muda wa kujirudi au kupona vizuri na kurudisha virutubisho hasa madini chuma na foleti, ambayo huitajika sana kwa ukuaji wa mtoto.

Kwa kitaalamu fistula hujulikana kama njia isiyo ya kawaida inayounganisha mfuko wa mkojo na uke, ambayo huruhusu mkojo na/au haja kubwa kutoka  bila kujizuia kwenye kuta za uke.

Nini hutokea?

Tatizo la kushindwa kujizuia kujikojolea na/au kupitisha haja kubwa kwenye tupu ya mwanamke linalojulikana kama fistula hutokea baada ya mwanamke kupata madhara kipindi cha kujifungua kutokana na kuwa kwenye uchungu wa kujifungua kwa muda mrefu (Prolonged and obstructed labor), kutokana na kichwa cha mtoto kushindwa kupita kwa urahisi kwenye tupu ya  mwanamke.

Hali hii husababisha tishu za kwenye tupu ya mwanamke, kibofu cha mkojo na puru (rectum), kugandamizwa kati ya kichwa cha mtoto na nyonga za mwanamke. Hii husababisha mfumo wa damu kwenye tishu hizi kuharibika na tishu kukosa damu na kuwa katika hali inayojulikana kitaalamu kama ischemic necrosis. Baadaye tundu hutokea kati ya tupu ya mwanamke na kibofu cha mkojo au kati ya tupu ya mwanamke na puru.

Matokeo yake ni mwanamke kutoa mkojo na/au haja kubwa bila kujizuia kupitia tupu yake (vagina).

Ukubwa wa tatizo

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linakadiria kuwa wasichana na wanawake wapatao millioni 4 duniani wanaishi na tatizo hili wakati kila mwaka wasichana na wanawake wengine 50,000 - 100,000 hupatwa na tatizo hili.

Fistula huonekana sana kwenye bara la Afrika na Asia ya kusini. Kwa Tanzania, wanawake na wasichana 1,200 kila mwaka hupatwa na tatizo hili. Katika tafiti mbili zilizofanyika Tanzania,

iliripotiwa kuwa wanawake walio katika umri kati ya miaka 22-24 ndiyo hupatwa na tatizo hili zaidi.

VVF husababishwa na nini?

  • Uchungu wa muda mrefu (Prolonged labour) ambao husababishwa na
    • Kutokuwa na usawa wa uwiano wa nyonga ya mama na ukubwa wa mtoto (CPD)
    • Mtoto kulala vibaya (malpresentation)
  • Upasuaji wa kuondoa kizazi (hysterectomy)
  • Upasuaji wa njia ya mkojo (repair of urethral diverticulum, electrocautery of bladder papilloma)
  • Upasuaji wa kansa za nyonga (pelvic carcinomas).

Dalili

  • Mkojo kutoka  bila kujizuia kwenye kuba ya uke ndio dalili muhimu
  • Kuna uwezekano wa kupata maambukizi hivyo dalili zifuatazo huweza kuambatana na dalili ya mwanzo homa na maumivu ya tumbo hasa ubavu na chini ya kitovu.

Vipimo

  • Majimaji yanatoka kwenye kuta za uke huchunguzwa vitu vifuatavyo:
    • Urea, creatinine, na potassium ili kuwa na uhakika kuwa ni VVF na sio Vaginitis (maambukizi ya uke)
    • Mkojo huoteshwa kuangalia kama kuna vimelea na kujua dawa gani yaweza kuvimaliza vimelea hivyo
  • Rangi ya indigo carmine hutolewa kwa njia ya mshipa na pindi inapoonekana ukeni huthibitisha VVF
  • Cystourethroscopy
  • Intravenous urogram

Matibabu

Kama tatizo limegundulika siku chache baada ya upasuaji mpira wa kukojolea (urinary catheter either transurethral or suprapubic) huwekwa kwa siku 30. Fistula ndogo (chini ya sentimita 1) huweza kupona yenyewe au kupungua.

Upasuaji ili kurekebisha VVF, aina za upasuaji

  • Vaginal approach
  • Abdominal approach
  • Electrocautery
  • Fibrin glue
  • Endoscopic closure using fibrin glue with or without adding bovine collagen
  • Laparascopic approach
  • Using interposition flaps or grafts

Baada ya upasuaji

  • Mgonjwa huwekewa Suprapubic catheter (mpira wa mkojo) kwa siku 6 hadi 60 ili kupunguza mvutano wa nyuzi
  • Vitamin C 500mg mara tatu kwa siku ili mkojo uwe wa asidi ili kuzuia maambukizi na kutengenezwa kwa mawe.
  • Tiba ya kichochezi cha ostrogeni kwa wakina mama walikwisha acha kupata siku zao (postmenopausal)
  • Dawa za kuzuia mshtuko wa mfuko wa mkojo-methylene blue na Atropine sulfate
  • Antibaotiki
  • Pumzisha nyonga kwa kuzuia tendo la ndoa kwa kipindi cha wiki 4 hadi 6. Ingawa wengine hushauri hadi miezi mitatu.

 

Swala hili limekuwa likiwatatiza wamama wengi wanaopatwa na tatizo la mimba kuharibika.

Ni vizuri kwanza kujua vitu vinavyoweza kusababisha mimba kuharibika.

Mimba nyingi huharibika kutokana na makosa ya ukuaji wa mtoto. Sehemu kubwa ya makosa haya huwa ni kwenye vinasaba vyake. Yanaweza kuwa ya kurithi au yasiyo ya kurithi yaliyotokea kwa bahati mbaya kwa mtoto.

Zipo pia sababu nyingine kama vile maumbile ya viuongo vya uzazi, magonjwa ya mama kama vile kisukari, magonjwa ya damu, magonjwa ya vijidudu (infection).

Pamoja na sababu za mimba kuharibika kuwa nyingi, mara nyingi linapotokea tatizo hili huwa sababu iliyosababisha haifahamiki. Hali hii husababisha akinamama wengi na wenza wao kubaki na maswali mengi kwanini imewatokea hivyo na hujiuliza kama inaweza kutokea tena kwenye ujauzito mwingine.

Mara nyingi hali hii hutokea mara moja na haijirudii. Hii ni kwa sababu makosa ya ukuaji yanayotokea bahati mbaya huwa ni jambo lenye uwezekano mdogo sana kujirudia. Hata hivyo iwapo ujauzito umeharibika kwa sababu nyingine kama vile za kimaumbile au magonjwa ya damu, uwezekano wa kujirudia huwa mkubwa iwapo hali hiyo haijagundulika na hatua stahiki kuchukuliwa.

Upungufu wa damu (anaemia) 

hutafsiriwa kama kupungua kwa kiwango cha hemoglobin katika damu damu chini ya kiwango kinachokubalika kiafya. Kiwango cha kawaida cha haemoglobin (Hb) katika mwili wa binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa kila mililita ya damu. Hata hivyo shirika la afya duniani (WHO) linatambua kiwango cha mpaka 11gm/mililita kuwa cha kawaida kwa mama mjamzito. Hivyo basi mjamzito mwenye kiwango chochote cha haemoglobin chini ya 11 gm/mililita hutafsiriwa kuwa na upungufu wa damu. Hata hivyo nchi nyingi hasa zinazoendelea hutambua kiwango cha mpaka gramu 10 kwa mililita kuwa ni upungufu wa damu kwa mjamzito.

Kwa mjamzito anayehudhuria kliniki kwa mara ya kwanza, upungufu wa damu kipindi cha ujauzito humaanisha kiwango cha hemoglobin chini ya <11.0 g/dL, na mimba inapofikisha wiki 28 upungufu wa damu hutambuliwa iwapo hemoglobin itashuka na kuwa chini ya 10.5 g/dL.

Kwa kuzingatia hilo, mama mjamzito hushauriwa kupima wingi wa damu siku anapohudhuria kliniki kwa mara ya kwanza na pindi mimba inapofikisha wiki 28.

Viwango vya Anaemia

Upungufu wa damu

unaweza kugawanywa katika viwango vikuu vinne, yaani upungufu wa damu wa kawaida (mild anaemia) ambao ni kati ya 9-11 gm/ml, upungufu wa damu wa kati (moderate anaemia) ambao ni kati ya 7-9 gm/ml, upungufu wa damu mkali (severe anaemia) ambao ni kati ya 4-7 gm/ml na upungufu wa damu mkali zaidi (very severe anaemia) ambao ni chini ya 4gm/ml.

Mzunguko wa madini ya chuma mwilini

Kwa kawaida mwili wa mwanamke huifadhi gramu 3.5 mpaka 4.5 za madini ya chuma. Asilimia 75 huifadhiwa kama hemoglobin katika chembe damu nyekundu, asilimia 20 kama ferritin katika mifupa na asilimia 5 inayobaki huifadhiwa katika misuli na vimeng’enyo vingine vya mwili.

Wanawake wasio wajawazito hupoteza karibu gramu 1 za madini ya chuma kutoka katika seli za mwili zinazokufa kila siku na gramu 1 zaidi kila siku wanayokuwa kwenye hedhi.

Hali ya tumbo kuuma wakati wa hedhi huitwa dysmenorrhea.

Zipo aina mbili za hali hii.

Aina ya kwanza ni maumivu yanayoanza tangu umri wa kuvunja ungo. Katika aina hii huwa hakuna ugonjwa unaosababisha uwepo wa haya maumivu. Hali hii hupona hata bila matibabu baada ya mizunguko kadhaa ya hedhi au baada ya kujifungua. Aina hii inaitwa primary dysmenorrhea (tuiite maumivu ya awali).

Aina ya pili mara nyingi hutokea miaka kadhaa baada ya kuvunja ungo. Aina hii husababishwa na ugonjwa wa viungo vya uzazi. Iwapo ugonjwa huo utatokea kabla msichana hajavunja ungo basi maumivu yanaweza kuanza kuanzia umri wa kuvunja ungo. Maumivu yaliyosababishwa na uwepo wa ugonjwa hayaponi bila kuutibia ugonjwa ulioyasababisha.

Magonjwa yanayoweza kusababisha maumivu ya hedhi ni fibroids, infection, uvimbe ndani ya kifuko cha uzazi (polyp) na ugonjwa unaoitwa endometriosis na adenomyosis. Ugonjwa wa endometriosis na adenomyosis upo Tanzania lakini hausikiki kwa sababu vituo vingi vya huduma havina vifaa vya kugundua uwepo wake. Nitaufafanua kwa kirefu kwenye topic yake.

Msichana au mwanamke mwenye maumivu ya hedhi anatakiwa kumuona daktari kwa ajili ya vipimo na ushauri wa matibabu.

Kuharibika kwa Mimba ni nini?

Utangulizi

Kuharibu/kuharibika kwa mimba kwa njia ya kutoa kiinitete (embryo) au mjusi (fetus) kabla ya kutimiza umri wa kuweza kuishi nje ya mfuko wa kizazi hujulikana kama abortion 1. Mimba inapoharibika yenyewe kabla ya kutimia umri wa wiki 20 hujulikana kama miscarriage.

Kuharibu mimba kwa kukusudia bila kuwepo kwa sababu za msingi za kitabibu zinazomruhusu mama mjamzito kufanya hivyo ndio hujulikana kama criminal abortion, ambayo kulingana na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kosa la jinai (Criminal Act).
Katika makala hii nitaeleza kwa kina kuhusu kuharibika kwa mimba. Karibia mimba milioni 56 huharibika kila mwaka duniani kote 2 .

Kuharibika kwa mimba miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito (First Trimester Miscarriage)

Visababishi

a) Asilimia 50-70% ya mimba zote zinazoharibika zenyewe wakati wa miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito hutokana na matatizo ya kiasili au vina saba (genetics or chromosome abnormalities) kama;

  • Autosomal trisomy (22.3%)
  • Monosomy (8.6%)
  • Triploidy (7.7%)
  • Tetraploidy (2.6%)

b) Magonjwa yanayotokana na kinga ya mwili (Collagen Vascular Disease)-Magonjwa haya hutokana na mwili wa binadamu kutengeneza chembechembe za antigen ambazo hushambulia viungo vyake venyewe . Magonjwa haya ni Systemic Lupus Erythematosus (SLE) na Antiphospholipid Antibody Syndrome.

  • Utafiti mpya unaonesha ya kwamba watoto wanaokunywa juisi au ambao mama zao walikunywa vitu vyenye sukari kipindi cha ujauzito wapo kwenye hatari kubwa ya kuugua ugonjwa wa Pumu
  • Wajawazito ambao walikunywa soda na vinywaji vyenye sukari (sugary beverages) wana asilimia 70 ya kuzaa watoto ambao baadae watapata ugonjwa wa Pumu

Matokeo ya utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani yameonyesha ya kwamba, watoto wanaokunywa vinywaji vyenye sukari au juisi (artificial juice) na ambao mama zao walikunywa soda kipindi cha ujauzito wao wapo kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa Pumu.

Watoto ambao waligundulika kuwa na kiwango kikubwa cha sukari aina ya fructose (ambayo hupatikana kwenye juisi au soda) kwenye milo yao kipindi cha ukuaji, walikuwa kwenye hatari ya asilimia 79 kupata ugonjwa wa Pumu ukilinganisha na watoto ambao hunywa vinywaji vyenye sukari kwa nadra au wale watoto ambao hawanywi kabisa vinywaji hivyo.

Kina mama ambao walitumia vinywaji vyenye sukari au soda kipindi cha ujauzito pia walikuwa kwenye hatari ya asilimia 70 kuzaa mtoto ambae baadae atagundulika kuwa na ugonjwa wa Pumu ikilinganishwa na kina mama ambao walitumia vinywaji vyenye sukari kwa nadra au ambao hawakutumia kabisa vinywaji hivyo kipindi cha ujauzito.

Tatizo la mimba kutoka au kutolewa ni jambo ambalo limewakumba kina mama wengi walio katika umri wa kuzaa. Aidha mijadala kuhusu kuhalalishwa au kuendelea kuharamishwa kwa utoaji mimba ni jambo linalochukua nafasi ya mazungumzo ya kila siku katika maisha yetu.

Kwa baadhi ya nchi, suala la utoaji mimba ni jambo lililohalallshwa kisheria ingawa kwa nchi kama Tanzania, suala hili halijahalalishwa isipokuwa tu pale panapokuwa na sababu za kitabibu zinazolazimisha kufanya hivyo.

Nini maana ya mimba kutoka?

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), utokaji mimba (abortion) hutokea pale ambapo kiumbe (mimba) kilicho chini ya wiki 22 kinapotoka kwa sababu moja ama nyingine, au kinapotolewa kwa njia yeyote ile. Aidha shirika la Afya limekwenda mbali zaidi na kutoa maana nyingine ya utokaji mimba kuwa ni pale mtoto (kiumbe) anapozaliwa akiwa na uzito wa chini ya gram 500.

Aidha baadhi ya matabibu hupendelea kutumia neno 'abortion' kumaanisha kitendo cha utoaji wa mimba kinachofanywa na mtu mwingine ama kwa njia sahihi au zisizo sahihi na 'miscarriage' kumaanisha kitendo cha mimba kutoka yenyewe kwa sababu nyingine yeyote. Ukiacha tofauti hizi za jinsi ya kuharibika kwa mimba, abortion na miscarriage humanisha kitu kilekile cha mimba kutoka.

Aina za utokaji/utoaji mimba (Classification of abortion)

Utokaji mimba umeanishwa katika aina zifuatazo:

Utokaji wa mimba wa hiyari yaani kitendo cha mimba kutoka yenyewe (spontaneous abortion)

  • Mimba inayotishia kutoka ingawa bado haijatoka (threatened abortion)
  • Utokaji wa mimba usioepukika (inevitable abortion)
  • Utokaji wa mimba ulio kamili (.co.tzplete abortion)
  • Utokaji wa mimba usio kamili (in.co.tzplete abortion)
  • Mimba iliyotoka bila kugundulika kuwa imetoka (missed abortion)
  • Utokaji wa mimba unaojirudia rudia (recurrent abortion)
  • Utoaji mimba kinyume cha sheria (illegal abortion)
  • Utoaji mimba kwa sababu za kiafya (therapeutic abortion)
Ukurasa 3 ya 5