Image

Magonjwa Yasiyo ambukizi(Non-Communicable Disease)

Ni moja kati ya magonjwa sugu ambayo sio ambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Vilevile ni kati ya magonjwa ambayo ni endelevu.

Kuna magonjwa makuu manne yasiyo ambukizi

 • Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu-shambulizi la moyo na kiharusi
 • Kansa au saratani
 • Kisukari
 • Magonjwa sugu yasababishayo kuziba mfumo wa upumuaji kitaalamu COPD’s

Kulingana na taarifa za shirika la afya duniani

 • Watu milioni 36 kila mwaka huathiriwa na magonjwa yasiyo ambukizi
 • Karibu asilimia 80 sawa na watu milioni 29 hufa kutokana na magonjwa yasiyo ambukizi katika nchi za vipato vidogo na vya kati.
 • Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu ndio husababisha vifo zaidi watu milioni 17 kwa mwaka, ikifuatiwa na kansa watu milioni 7, mfumo wa upumuaji watu milioni 4, na kisukari milioni 1.
 • Magonjwa haya yote huweza kusababishwa na vifuatavyo: utumiaji wa tumbaku, kutofanya mazoezi kabisa, utumiaji wa pombe kupita kiasi, utumiaji wa vyakula visivyo bora.

Je magonjwa haya yanaathari gani kijamii na kiiuchumi?

Magonjwa haya yanaelekea kukwamisha malengo ya umoja wa taifa ya maendeleo ya milenia. Na kwasasa kuna uhusiano wa karibu kati ya umaskini na magonjwa yasiyoambukizi. Kuna uzorotaji wa juhudi za kupunguza umaskini kwasababu ya ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukizi .

 • Mazingira magumu husabisha watu wa kipato cha chini kuumwa zaidi na kufa mapema kuliko wa kipato cha juu, kwasababu hao ndio huweza kupelekea kuwa karibu  na bidhaa zenye madhara kama tumbaku, chakula kischo bora na kutoweza kumudu huduma za afya. Umaskini huweza kuingia haraka kama magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, kansa, kisukari na Magonjwa sugu yasababishayo kuziba mfumo wa upumuaji kitaalamu COPD’s yakivamia familia zisizo na uwezo kwasababu ya kuwa na rasilimali chache kwa ajili ya gharama za huduma ya afya.

Jinsi ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasioambukizi

 • Hapa mbinu elekezi huitajika hasa kwa kushirikisha sekta mabalimbali zikiwemo ya afya, elimu, fedha, na mipango ilikuzuia na kudhibiti magonjwa haya.
 • Cha muhimu kingine ni kupunguza vihatarishi ambavyo hupelekea kwenye magonjwa haya:
  • Kupunguza matumizi ya tumbaku
  • Kula chakula bora
  • Kufanya mazoezi
  • Kupunguza kunywa pombe
  • Elimu ya afya ya msingi itasaidia kugundulika na kutibiwa mapema kwa magonjwa haya
  • Njia nyingine ni kukuza uelewa kuhusu kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukizi kwa kuanzisha sera ya afya ya umma.

Kwa ufupi kwasasa kuna mlipuko wa magonjwa yasiyoambukizi hata hapa Nchini kwetu Tanzania, ni muhimu kuzingatia : mazoezi japo nusu saa kwa siku, kula chakula bora, kupunguza matumizi ya tumbaku na unywaji wa pombe. 

Imesomwa mara 21182 Imehaririwa Jumatatu, 17 Desemba 2018 19:53
Dr.Mayala

Dr.Henry A Mayala ni daktari bingwa Wa Tiba ya moyo katika taasisi ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI), ambaye kwasasa anasomea shahada ya uzamivu (PhD) ya Tiba ya Moyo katika Chuo Kikuu cha Tongji  nchini China.

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Makala shabihana