Kiharusi ni hali ya kuziba (ischemic) au kupasuka (hemorrhagic) kwa mishipa ya damu ya ubongo na kisha kupelekea ku ‘paralize’ au kifo. Kuna wakati ububu, uziwi, upofu hutokana na kiharusi.
Asilimia 85 ya kiharusi hutokana na kuziba kwa mishipa ya damu (ISCHEMIC STROKE). Aina ya pili ambayo hutokea kwa asilimia 15, hutokana na kupasuka kwa mishipa ya damu ya kwenye ubongo, kitaalamu hujulikana kama (HEMORRHAGIC STROKE); ni mbaya sana na mara nyingi hupelekea kifo.
Vihatarishi vyake
Kiharusi kinaweza kumpata mtu yeyote yule lakini wafuatao wana uwezekano Zaidi wa kupata kiharusi.
- Mwenye historia ya kiharusi kwenye familia yake
- Mwenye kisukari ambacho hakijathibitiwa
- Mwenye shinikizo la damu (BP) ambayo halijathibitiwa
- Mwenye maradhi ya mishipa ya damu ya ubongo, au maradhi ya moyo
- Mwenye maradhi ya kukosa usingizi
- Mwenye cholesterol nyingi, mnene wa kupindukia, Kutofanya mazoezi
- Uvutaji wa sigara na Unywaji pombe
- Utumiaji wa madawa ya kulevya
Dalili zake
- Kushindwa kuongea au kutamka maneno sawasawa
- Kupinda uso na kushindwa kutumia mkono ama mguu
- Kizunguzungu na kukosa balance
- Kutokuona vizuri
- Kichwa kuuma
Matibabu yake
Kuwahi haraka hospitali kitengo cha dharura ndani ya saa 24 ili kupewa dawa ya kushusha shinikizo la damu na ubongo, na za kuzuiza kifafa; kisha kufanya vipimo vya kichwa yaani CT scan au MRI, na ultrasound.
Madaktari na wauguzi watakushauri kuhusu kuanza matibabu ya haraka ya kuzibua mishipa ya damu (Angiosuite) au kuondoa donge la damu kwa upasuaji (Theathre).
Baada ya kudhibiti hali ya dharura, utashauriwa kuanza mazoezi tiba (physiotherapy) pamoja na kuwaona jopo maalum la madaktari wa kiharusi.