Tezi Dume (Prostate gland)
Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).
Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa tabu.
Kuvimba Tezi Dume (BPH)
Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu huitwa Benign Prostate Hyperplasia au wengine hupenda kutumia maneno Benign Prostate Hypertrophy kwa kifupi BPH. Kwenye makala hii tutautumia sana ufupisho huu wa BPH ili kurahisisha mambo.
Ukuaji wa tezi dume hupitia hatua kuu mbili. Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi dume linapoongezeka ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo ukuaji husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka 25 hadi 30 ndipo hatua ya pili ya ukuaji huanza tena. Ukuaji huendelea kwa viwango na kasi tofauti kati ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha BPH katika umri wa utu uzima.
Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando wa tishu unaozulizunguka hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea kukua, hufikia wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu. Hali hii husababisha kibofu cha mkojo kuwa na ngozi ngumu. Hali hii hufanya kibofu cha mkojo kuhisi kutaka kutoa mkojo nje hata kama kiasi cha mkojo ndani yake ni kidogo sana. Hufikia wakati, kibofu huwa dhaifu na kupoteza uwezo wake wa kuhisi kutoa mkojo na hivyo kufanya mtu anapokojoa kushindwa kutoa mkojo wote na badala yake hubakiza kiasi fulani cha mkojo kwenye kibofu.
Ukimwi “upungufu wa kinga mwili”, ni ugonjwa unaoshambulia na kuua chembe chembe nyeupe za damu zinazosaidia mwili kupambana na magonjwa. Kutokana na upungufu huu wa kinga, magonjwa nyemelezi huanza kumpata muathirika wa ukimwi. Magonjwa yatokanayo na ukimwi uweza kujidhihirisha sehemu mbali mbali za mwili ikiwemo eneo la kinywa na uso. Kwa sasa nitaandika juu ya magonjwa ya eneo la kinywa na uso.
Fangasi za mdomoni (oral candidiasis)
Ugonjwa huu hujidhihirisha kama utando mweupe kwenye ulimi, paa la kinywa au kuta za kinywa, utando huu ni rahisi kukwanguliwa na kuacha ngozi laini yenye vipele vipele vyekundu. Wakati mwingine uonekana kama vipele vipele vyeupe kwenye kinywa.
Matibabu
Ugonjwa huu hutibika kwa kutumia dawa za kawaida za fangasi, ziwe vidonge, za maji au za kumun’gunya katika hali ya gel
fangasi kwenye paa la kinywa
Moja ya magonjwa hatari sana ambayo yanaweza kumpata mtu yoyote ni ugonjwa wa shambulizi la moyo. Huu ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanaume na wanawake.
Kwa kawaida, ugonjwa huu hutokea pale ambapo sehemu ya nyama ya moyo inapoharibika au kufa kutokana na kukosa damu ya kutosha.
Je tatizo hili husababishwa na nini?
Husababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu inayosambaza damu katika moyo (coronary artery blockage) kutokana na mafuta mabaya mwilini (atherosclerotic plaque).
Watu gani wapo katika hatari ya tatizo hili?
Watu walio katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa huu ni pamoja na
- Wenye umri mkubwa miaka 45 kwa wanaume na 55 kwa wanawake
- Wavutaji wa sigara
- Watu wenye mafuta ya lijamu katika damu au wale wenye mafuta mabaya aina ya triglycerides na low density lipoprotein kwa kiwango kikubwa katika damu zao
- Wenye kisukari
- Wenye matatizo ya shinikizo la damu
- Walio na unene kupita kiasi (obesity)
- Wenye matatizo sugu ya kushindwa kufanya kazi kwa figo zao (chronic renal failure)
- Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)
- Wanywaji wa pombe kupindukia
- Watumiaji wa madawa ya kulevya hasa cocaine na methamphetamine
- Watu wenye msongo wa mawazo (Chronic high stress levels)
- Upungufu wa vitamin B2, B6, B12 na folic acid
Dalili za shambulizi la moyo
- Maumivu makali ya ghafla kifuani ambayo husambaa kwenye taya, shingo, bega na mkono wa kushoto
- Kupumua kwa shida
- Kutoka jasho kwa wingi sana (diaphoresis)
- Kuhisi mapigo ya moyo yanapiga haraka (palpitations)
- Kichefuchefu
- Kutapika
- Kuchoka haraka sana
- Kupoteza fahamu
Shambulizi la moyo limehusishwa na nini?
Tafiti mbalimbali zimeusisha mambo yafuatayo na shambulizi la moyo
- Msongo wa mawazo
- Maambukizi hasa vichomi vinavyosababishwa na vimelea vya chlamydophila pneumonia.
- Hutokea zaidi asubuhi hasa saa tatu (saa 3 asubuhi)
Vipimo na uchunguzi
- ECG - Kipimo hiki huonyesha ni sehemu gani ya moyo iliyoathirika
- Coronary angiography - Kinasaidia kwa kuangalia wapi ambapo mishipa ya damu imekuwa membamba sana kupita kiasi (narrowing of vessels) au imeziba.
- Cardiac markers levels
- X-ray ya kifua (chest X-ray)
- MPI (Myocardial Perfusion Imaging) - Kipimo hiki hufanywa kwa kutumia mashine maalum ya PET Scan ambapo kinauwezo wa kugundua tatizo la shambulizi la moyo, huchunguza kikamilifu maumivu ya kifua, huangalia mwelekeo wa tiba ya kuzuia damu kuganda, hutoa mwelekeo wa ugonjwa wa shambulizi la moyo kama ni mzuri au mbaya, hutathmini ubora wa tiba ya shambulizi la moyo kabla na baada ya mgonjwa kupata tiba, huweza kutambua hata shambulizi la moyo ambalo si rahisi kugundulika kwa kutumia vipimo vyengine na pia hutathmini ukubwa wa tatizo la shambulizi la moyo. Hata hivyo kwa sasa kipimo hiki hakipatikani nchini kwetu.
Ili kuweza kutambua uwepo wa tatizo hili, mwaka 1979, shirika la Afya Duniani (WHO) liliweka vigezo vya kutambua shambulizi la moyo.
Vigezo hivyo ni
- Historia ya kuwa na maumivu ya kifua zaidi ya dakika 20
- Mabadiliko katika kipimo cha ECG, na
- Kupanda na kushuka kwa kipimo kiitwacho kitaalamu cardiac biomarkers hasa creatine kinase - MB na troponin
Matibabu
Shambulio la moyo ni tatizo linalohitaji matibabu ya dharua. Lisipotibiwa kwa haraka husababisha kifo katika muda mfupi sana tangu mgonjwa apatwe na tatizo. Matibabu ya tatizo hili hujumuisha
- Kumpa mgonjwa hewa ya oksijeni
- Mgonjwa hupewa vidonge vya Aspirini ndogo kuzuia damu kuganda (thrombolytic) kwa ajili ya kuyeyusha damu iliyaganda na hivyo kuzibua mirija midogo ya damu katika moyo iliyozibwa na kuganda huku kwa damu.
- Vile vile mgonjwa hupewa dawa za kuweka chini ya ulimi kiitwacho nitrogylycerin (glyceryl trinitrate) ambazo husaidia kutanua mishipa ya damu (vasodilation)
- Dawa ya kutuliza maumivu kwa mfano morphine
- Dawa ya kuyeyusha mafuta katika mishipa ya damu kama vile clopidogrel
- Kuzibua mishipa ya damu inayosambaza damu katika moyo kwa kutumia - Percutaneous coronary intervention (PCI)
- Upasuaji (CABG)
Njia za kuzuia shambulizi la moyo
- Kuacha kuvuta sigara
- Kufanya mazoezi ya mara kwa mara
- Kupunguza unywaji wa pombe
- Kubadilisha aina ya mlo. Kupunguza mafuta katika mlo na chumvi.
- Kutumia mafuta ya samaki (omega-3 fatty acids)
- Kuna utafiti unaosema kuwa uchangiaji damu hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo hasa kwa wanaume.
Madhara ya shambulizi la moyo
- Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)
- Matatizo katika mfumo wa mapigo ya moyo (Atrial fibrillation) ambayo hatimaye hupelekea kifo
- Shambulizi la moyo kurudia mara ya pili
- Kifo cha ghafla (sudden death)
Utangulizi
Figo ni miongoni mwa viungo muhimu sana katika mfumo wa utendaji kazi wa mwili wa binadamu. Kwa kawaida, mwili wa binadamu una figo mbili zenye maumbo yanayofanana kama yale ya maharage, yakiwa yamejificha nje ya utando unaozunguka tumbo, chini kidogo ya mbavu za chini.
Kazi za figo
Kazi kuu za figo ni kuchuja vitu mbalimbali pamoja na sumu kadhaa katika damu na hivyo kusaidia katika kuhifadhi na kuthibiti kiwango cha maji na madini (electrolytes) mwilini. Katika kutekeleza hayo, figo huchuja vitu hivyo pamoja na maji yaliyo mwilini na kutengeneza mkojo, huchuja pia maji yasiyohitajika mwilini huku yakinyonya madini na kemikali muhimu kuzirudisha katika mzunguko wa damu na kutoa nje uchafu usiohitajika.
Kazi nyingine za figo ni
- Kurekebisha na kuthibiti kiasi cha vitu mbalimbali katika damu pamoja na kiasi cha maji katika mwili
- Husaidia kutengeneza kiasili cha erythropoietin ambacho ni muhimu sana katika utengenezaji wa chembe nyekundu za damu.
- Husaidia uzalishaji wa vitamini D
- Husaidia pia katika kuthibiti na kurekebisha shinikizo la damu mwilini (blood pressure)
Utengenezaji wa mkojo
Kwa kawaida damu inayozunguka mwilini hatimaye huingia kwenye figo kwa ajili ya kuchujwa, kutoa uchafu pamoja na sumu nyingine zisizohitajika mwilini. Kitendo hiki cha utengenezaji mkojo hufanyika katika hatua kuu zifuatazo;
- Hatua ya kwanza ni uchujaji. Damu kutoka nje huingia ndani ya mafigo na kupita kwenye glomeruli, lenye umbo kama chekeche/chujio ambalo limeundwa na mishipa mingi midogo ya damu iliyojizungusha pamoja. Vitu mbali mbali, maji pamoja na sumu zilizo katika damu inayopita kwenye vimishipa hivi na kisha kuingia katika mirija mingine mikubwa kwa ajili ya uchujaji zaidi.
- Mirija inayofuata huendelea kuchuja damu na kunyonya baadhi ya vitu vilivyo chujwa kimakosa kuvirudisha mwilini, mpaka kiasi sahihi cha uchafu kinachotakiwa kuchujwa kinapokuwa kimefikiwa.
- Mara baada ya mkojo kutengenezwa na kutolewa kwenye figo, husafiri kuingia kwenye kibofu cha mkojo kwa kupita kwenye mirija ijulikanayo kama ureta. Kutoka kwenye kibofu, mkojo hutolewa nje ya mwili kupitia kwenye mrija wa urethra.
Figo kushindwa kufanya kazi (Renal Failure/ Kidney Failure)
Kushindwa kufanya kazi kwa figo hutokea iwapo sehemu ya figo au figo lote litapoteza uwezo wake wa kuchuja maji na uchafu kutoka katika damu na kutengeneza mkojo. Kitendo hiki husababisha kusanyiko la uchafu pamoja na sumu kadhaa katika damu ambazo ni hatari kwa afya ya mhusika.
Aina za figo kushindwa kufanya kazi
Figo kushindwa kufanya kazi kumeganyika katika makundi yafuatayo
- Figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla (Acute Renal Failure (ARF) au Acute Kidney Failure (AKF).
- Figo kushindwa kufanya kazi kwa kiasi (Mild renal/kidney insufficiency)
- Tatizo sugu la figo kushindwa kufanya kazi (Chronic renal failure)
Figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla (Acute Renal Failure (ARF)
Hii ni hali inayotokea kwa ghafla, na kudumu kwa saa chache mpaka siku chini ya 14, na kusababisha ongezeko la kiwango cha creatinine na urea katika damu. Hali hii huwapata karibu asilimia 5% ya wagonjwa waliolazwa hospitali kwa sababu ya matatizo mbalimbali. Aidha hali hii hutokea zaidi kwa wagonjwa mahututi na wale wanaohitaji uangalizi wa kipekee, yaani waliolazwa ICU.
Katika makala hii tutatumia zaidi kifupisho cha ARF.
Visababishi na aina za ARF
Visababishi (au aina) vya ARF vinaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu:
- Matatizo yanayoathiri mtiririko wa damu kabla ya kuingia katika figo (Prerenal causes/failure)
- Matatizo ndani ya figo lenyewe yanayozuia na kuathiri uchujaji wa damu au uzalishaji wa mkojo (Renal causes/failure)
- Matatizo yanayoathiri mtiririko wa mkojo nje ya figo (Postrenal causes/failure)
Matatizo yanayoathiri mtiririko wa damu kabla ya kuingia katika figo (Prerenal causes/failure)
Aina hii hutokea kwa takribani asilimia 60 mpaka 70 ya ARF zote. Katika kundi hili, figo hukosa damu ya kutosha kwa ajili ya kuchuja na hatimaye hushindwa kufanya kazi yake ipasavyo. Mambo yanayoweza kusababisha prerenal failure ni pamoja na:
- Upungufu wa maji mwili unaosababishwa na kutapika kupita kiasi, kuharisha, au kupoteza damu kupita kiasi (kwa sababu ya ajali au kuumia)
- Kuvurugika kwa mtiririko wa damu inayoingia kwenye figo kwa sababu ya:
- Kushuka kwa ghafla kwa shinikizo la damu kwa sababu ya kupoteza damu nyingi wakati wa upasuaji mkubwa, kuumia au kuungua sehemu kubwa ya mwili, au maambukizi katika mfumo wa damu (sepsis) yanayoweza kufanya mishipa ya damu kutanuka na kushusha shinikizo la damu
- Kuziba au kusinyaa kwa mishipa inayopeleka damu kwenye figo
- Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure) au shambulio la moyo (heart attack) linalosababisha kushuka kwa shinikizo la damu
- Ini kushindwa kufanya kazi (liver failure) kunakoweza kusababisha mabadiliko katika mfumo wa homoni zinazoathiri shinikizo la damu pamoja na mtiririko wa damu kwenda kwenye figo.
Mwanzoni kabisa mwa pre-renal failure huwa hakuna athari yoyote inayotokea kwenye figo, na mara nyingi, figo laweza kurudi katika hali yake ya kawaida iwapo chanzo cha tatizo kitagunduliwa na kushughulikiwa ipasavyo.
Matatizo ndani ya figo lenyewe yanayozuia na kuathiri uchujaji wa damu au uzalishaji wa mkojo (Renal causes/failure)
Mambo yanayosababisha madhara katika figo husababaisha karibu asilimia 25 mpaka 40 ya vyanzo vyote vya ARF. Visababishi vilivyo katika kundi hili hujumuisha vile vinavyoathiri uchujaji, mtiririko wa damu ndani ya figo na seli za figo zinazoshughulika na uchujaji na ufyonzaji wa chumvi na maji.
Visababishi hivyo ni pamoja na:
- Magonjwa katika mishipa ya damu
- Kuwepo kwa damu iliyoganda ndani ya mishipa ya damu inayopita katika figo
- Ajali/Kuharibika kwa tishu na seli za figo
- Magonjwa ya mzio katika glomeruli na figo kwa ujumla (glomerulonephritis). Magonjwa yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja na maambukizi (infection) ya bacteria jamii ya streptococci.
- Magonjwa ya mzio katika nyama za figo (acute interstitial nepthritis). Mambo yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja na matumizi ya baadhi ya madawa kama vile Aspirin, Ibuprofen (Brufen), baadhi ya antibiotics, na baadhi ya dawa za kutoa maji mwilini (antidiuretics); magonjwa kama vile saratani ya damu (leukemia), lupus na lymphoma. Magonjwa ya mzio katika nyama za figo husababisha madhara katika seli zinazohusika na uchujaji na ufynzaji wa chumvi na maji.
- Magonjwa ya ukosefu wa damu katika mirija ya figo (acute tubular necrosis) ambayo hufanya seli na tishu za mirija hii kufa na hivyo mirija kushindwa kufyonza chumvi na maji kuyarudisha mwilini. Mambo yanayosababisha hali hii ni pamoja na shock (upungufu wa damu kuingia kwenye figo), matumizi ya madawa kama vile baadhi ya antibiotiki, sumu, dawa zinazotumika viwandani na kwenye x-rays na baadhi ya madawa yanayotumika kutibu saratani.
Matatizo yanayoathiri mtiririko wa mkojo nje ya figo (Postrenal causes/failure)
Mambo yanayosababisha hali hii huchangia kati ya silimia 5 mpaka 10 ya vyanzo vyote vya ARF. Postrenal failure wakati mwingine huitwa pia obstructive renal failure kwa sababu husababishwa na mambo yanayozuia utoaji wa mkojo nje ya figo.
Kuziba kwa ureta moja ama zote mbili kunaweza kusababishwa na:
- Vijiwe figo (renal stones)
- Saratani ya viungo vya njia ya mkojo au viungo vilivyo karibu na njia ya mkojo kiasi cha kuzuia mkojo kutoka nje ya figo
- Matumizi ya baadhi ya madawa
Kuziba kwa njia ya mkojo katika eneo la kibofu cha mkojo kunaweza kutokana na:
- Kijiwe kibofu (bladder stone)
- Kuvimba kwa tezi dume (hii ni kwa wanaume)
- Kuwepo kwa damu iliyoganda katika kibofu
- Saratani ya kibofu cha mkojo
- Matatizo ya mfumo wa fahamu yanayoathiri utendaji kazi wa kibofu cha mkojo
Tafsiri nyingine ya ARF
Wagonjwa wa ARF wanaweza kupata mkojo kidogo sana au wasipate kabisa., au wanaweza kuwa na ongezeko la creatinine kwa kasi ya kutisha au kwa kasi ndogo sana. Hali hizi zinaweza pia kutumika kutoa tafsiri nyingine ya maana ya ARF.
Mtu anayetoa kiasi cha mkojo chini ya 400mL kwa siku hujulikana kama ana oliguria, na huchukuliwa kuwa ana hali mbaya ya kutoweza kupona.
Mtu anayetoa mkojo chini ya 100mLkwa siku husemwa ana Anuria, ambayo kama imetokea ghafla, huashiria kuwepo kwa tatizo la kuziba kwa mirija inayotoa mkojo kwenye figo zote mbili, na mara niyingi hali hii ni ya hatari zaidi. Tafsiri hii husaidia sana katika kuamua aina ya matibabu na muda wa kumpatia mgonjwa matibabu ili kuepusha madhara zaidi yanayoweza kumpata.
Dalili za ARF
Katika hatua za mwanzo mwanzo, baadhi ya waathirika wanaweza wasioneshe dalili zozote za tatizo hili. Dalili ni kama
- Kupungua kwa uzalishaji mkojo
- Kuvimba mwili
- Kupoteza umakini
- kuchanganyikiwa
- Uchovu
- Kulegea mwili
- Kichefuchefu na kutapika
- Kuharisha
- Maumivu ya tumbo
- Kuhisi ladha ya chuma na uchachu mdomoni
- Na katika hatua za mwisho kabisa, mgonjwa anaweza kupata degedege na hatimaye kupoteza fahamu (coma).
Vipimo na uchunguzi
Kama ilivyoainishwa hapo juu kuwa baadhi ya wagonjwa wanaweza wasiwe na dalili zozote za tatizo hili. Hata wale wenye kuonesha dalili, zinaweza zisiwe mahsusi (non-specific). Uchunguzi wa mwili unaweza usioneshe tatizo lolote lile, au kukawa na dalili chache sana ambazo zinaweza zisimsaidie sana daktari kufikia uamuzi.
Baadhi ya vipimo vinavyoweza kugundua uwepo wa ARF ni pamoja na
- Kipimo cha utendaji kazi wa figo (Renal function tests) ambacho husaidia kuchunguza kiwango cha urea (blood urea nitrogen (BUN) katika damu. Aidha husaidia pia kuchunguza ongezeko la kiwango cha creatinine katika damu.
- Uchunguzi wa kiwango cha madini mbalimbali katika damu (blood electrolytes)
- Uchunguzi wa damu (Full Blood Picture): Husaidia kuonesha uwepo wa maambukizi ya bacteria na/au upungufu wa damu mwilini (anaemia)
- Kupima kiasi cha mkojo kinachotolewa na mgonjwa katika masaa 24
- Uchunguzi wa mkojo (Urine analysis): Rangi ya mkojo, kiasi cha electrolytes, uwepo wa usaha au damu au casts.
- Ultrasound ya figo na kibofu cha mkojo
- Renal biopsy.
Matibabu ya ARF
Matibabu ya ARF hutegemea kwanza chanzo chake na pili ukubwa wa tatizo. Kujua chanzo cha tatizo husaidia kufahamu ni aina gani ya matibabu yanayohitajika wakati kufahamu ukubwa wa tatizo huathiri uchaguzi wa aina ya matibabu na hata hitaji la kufanya dialysis. Hata hivyo inashauriwa sana kumpeleka mgonjwa kwa daktari bingwa wa magonjwa ya figo (nephrologist) kwa matibabu zaidi.
Kulingana na chanzo cha ARF, baadhi ya matibabu yanayoweza kufanyika, hutolewa yakiwa na lengo la:
- Kurekebisha kiasi cha upotevu wa maji mwilini ambapo mgonjwa hupewa i.v fluids pamoja kurekebisha kiasi cha madini (electrolytes) kilichopotea
- Kupunguza au kuzuia ongezeko la maji kwa wagonjwa ambao figo zao zimeshindwa kabisa kutoa maji nje ya mwili
- Kuongeza uwezo wa moyo kufanya kazi vizuri au kuongeza shinikizo la damu husaidia kuongeza mtiririko wa damu kwenda kwenye figo
- Kurekebisha kiasi cha madini mwilini kitendo ambacho husaidia mwili kufanya kazi zake vema
Dialysis
Iwapo pamoja na matibabu hayo, figo za mgonjwa zinaendelea kudorora, mgonjwa hana budi kufanyiwa dialysis. Dialysis ni kitendo cha kutoa uchafu na maji yasiyohitajika katika damu. Kitendo hiki hufanywa kwa kupitia mishipa ya damu iliyo chini ya ngozi (hemodialysis) au kwa kupitia tumboni (peritoneal dialysis). Katika hemodialysis mirija hii huunganiswa kwenye mashine ambayo hufanya kazi kama figo. Damu kutoka kwa mgonjwa huingia katika mashine kisha huchujwa ili kuondoa sumu, uchafu pamoja na maji yasiyohitajika kabla ya kurejeshwa tena mwilini.
Kitendo hiki hufanyika angalau mara mbili mpaka tatu kwa wiki, na kwa kiasi fulani ni ghali na si watu wote wa kipato cha chini wanaoweza kumudu gharama zake.
Katika peritoneal dialysis, uchafu pamoja na maji kutoka katika mzunguko wa damu huingia katika nafasi inayotenganisha tumbo na utando wake (peritoneal space), huchujwa kwenye utando huo kisha hutolewa kupitia sindano maalum (catheter ) iliyowekwa juu ya ngozi na kuingia ndani ya tumbo (peritoneal cavity).
Matarajio
Wagonjwa wengi wenye ARF hupona bila hata kuhitaji dialysis mara tu chanzo cha tatizo kinapogundulika na kushughuikiwa mapema. Hata hivyo wakati mwingine, pamoja na matibabu, baadhi ya figo hushindwa kurudia kufanya kazi kwa ufanisi wake wa awali. Watu kama hawa hawa wanahitaji kufuatiliwa kwa ukaribu na umakini mkubwa.
Kinga ya ARF
Inashauriwa
- kufanya uchunguzi wa figo walau mara moja kila mwaka. Hii husaidia kuchunguza utendaji wa figo na hivyo kuepuka madhara kabla hayajatokea.
- Kunywa maji kwa wingi ili kuyafanya mafigo yatende kazi zake kwa ufanisi.
- Kuepuka matumizi ya vitu ama madawa yanayoweza kuathiri nyama, seli au tishu za figo. Ni vema kutumia dawa pale tu unaposhauriwa na daktari.
- Watu wenye hatari ya kupata tatizo sugu la kushindwa kufanya kazi kwa figo (Chronic Renal Failure) wanashauriwa kufanya vipimo na cuhunguzi mara kwa mara
- Muone mtaalamu wa afya mara tu uonapo dalili za kuwepo kwa shida katika kukojoa au uonapo damu katika mkojo
Ugonjwa wa Trichomoniasis ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya jamii ya protozoan vinavyojulikana kama Trichomonas vaginalis. Ugonjwa huu huathiri mrija wa kupitisha mkojo unaojulikana kama urethra na tupu ya mwanamke (vagina). Trichomoniasis pia hujulikana kwa majina mengine kama Trichomonas vaginitis au Trich (tamka “Trick”).
Trichomoniasis huathiri watu milioni 8 kwa mwaka Nchini Marekani na watu milioni 170 kwa mwaka dunia nzima. Ugonjwa huu huonekana sana kwa wanawake kuliko wanaume labda kutokana na wanaume kutoonyesha dalili zozote wakati wa maambukizi au kutokana na majimaji ya kwenye tezi dume kuwa na madini ya zinc ambayo huathiri vimelea hivi vya Trichomonas vaginalis. Ugonjwa huu hupatikana kwa njia ya kujamiana bila kutumia kinga na mtu aliyeathirika na Trichomoniasis.
Nakumbuka mwanajumuiya mmoja wa TanzMed aliuliza swali na hapa naomba ninukuu “madaktari, poleni na kazi za kila siku. mimi nina tatizo napata sana hizi yellowish discharge au niseme kama rangi ya maziwa hivi zinatoka huku chini kwenye tupu, asubuhi, mchana na jioni kama dose ya panadol. lakini hazina harufu kabisa, maana nilisoma makala zenu inasema kama zinatoa harufu ni dalili ya infections. Halafu za kwangu ni nzito hasa na zinavutika. Naomba msaada wenu sijui itakuwa ni nini?” mwisho wa nukuu.
Katika jibu langu nilimuahidi kuendelea na makala za magonjwa ya zinaa na leo naendelea na sehemu hii ya nne.
Nini hutokea wakati wa maambukizi/Pathofiziolojia ya ugonjwa (Pathophysiology)
Umbile la vimelea vya Trichomonas vaginalis ni sawa na chembechembe moja ya damu nyeupe kwa upana (10 μm) ingawa wakati mwingine ukubwa waweza kutofautiana kulingana na mazingira. Kutokana kuwepo kwa mfano wa mikono kwa nje inayojulikana kama flagellum ambayo husaidia vimelea hivi kuingia kwenye tishu za mrija wa kupitisha mkojo pamoja na tupu ya mwanamke na hivyo kuharibu seli aina ya epithelium na kusababisha vidonda (microulcerations) katika tishu hizi. Hii ndiyo sababu kubwa ya kwanini watu wanaopata ugonjwa huu wako kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa ukimwi (HIV) na magonjwa mengine.
Wagonjwa huwa na dalili zipi?
Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) husababishwa na vimelea kitaalamu hujulikana E. Coli. Vimelea hawa huishi huishi kwenye mfumo wa chakula bila kuleta madhara yoyote wawapo humo, ila wakiingia kwenye njia ya mkojo huleta maambukizi na kusababishwa ugonjwa wa UTI.
Kutokana na sababu za kimaumbile, Wanawake huathirika zaidi na ugonjwa wa UTI kuliko wanamume, hii ni kwa kwasababu kuna ukaribu zaidi katika njia hizi mbili za chakula na mkojo. Na pale mtu anaponawa baada ya haja kubwa ni rahisi zaidi kuhamisha vimelea hivi vya E. Coli kwenye njia ya mkojo pale ambapo hujifuta kuelekea mbele. Na ndiyo sababu, kwa wanawake, hushauriwa kunawa kuanzia mbele kuja nyuma. Endapo utanawa kuanzia nyuma kuja mbele, kuna uwezekano wa kuhamisha vimelea hivi ambavyo husambaa hadi kwenye kibofu, na endapo hautotibiwa vyema, basi hupanda hadi kwenye figo.
Pia, Wanawake huathiriwa sana na UTI kwa sababu wana njia fupi ya mirija ya mkojo (urethra) ambayo, inawapa bakteria wa UTI urahisi wa kusafiri hadi kwenye kibofu cha mkojo. Kujamiiana pia kunaweza kunaweza kupelekea kupata bakteria wanaosababisha UTI. Matumizi ya vipandikizi vya kuzuia mimba vinavyowekwa kwenye shingo ya uzazi huongeza hatari ya kupata UTI. Magonjwa kama kisukari na matatizo ya kimaumbile katika mfumo wa mkojo huongeza asilimia za kupata UTI.
Dalili za maambukizi ya njia ya mkojo
- Maumivu wakati wa haja ndogo, na hisia ya mkojo kuchoma choma
- Kubanwa na mkojo mara kwa mara
- Maumivu ya kiuno na maumivu ya chini ya kitovu
- Mkojo wa njano sana, na muda mwingine unatoa harufu
- Uchovu
- Homa
- Kuna baadhi ya watu hawawi na dalili yoyote (asymptomatic bacteriuria)
- Kukosa hamu ya kula,Kichefuchefu na kutapika.
Miongoni mwa magonjwa sugu yanayoendelea kuathiri afya za mamilioni ya watu wa nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania ni ugonjwa wa kisukari. Ugonjwa huu hutokea pale ambapo tezi kongosho linaposhindwa kutengeneza kichocheo aina ya Insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho cha insulin na kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha sukari kwenye damu au hyperglycemia.
Aina za Kisukari
Kisukari kimeanishwa katika makundi yafuatayo
Aina ya kwanza ya Kisukari au Type 1 Diabetes Mellitus
Hii ni aina ya kisukari inayowaathiri zaidi watoto na vijana (young adults).
Aina hii hutokea iwapo seli maalum zinazotengeneza homoni ya insulin zijulikanazo kama beta cells of Islet of Langerhans katika tezi kongosho zitakosekana au zitaharibika kwa sababu yeyote ile, na hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.
Upungufu wa akili ni tatizo ambalo kwa ujumla hutokea kabla ya mtu kuwa mkubwa (adulthood) na huambatana na dalili za kupunguwa uwezo wa akili ya utambuzi na kutafakari (cognitive functions) pamoja na kushindwa kukua kwa tabia za kuendana na mazingira yanayomzunguka mtu (adaptive behavior). Pia kitaalamu, upungufu wa akili hujulikana kama mtu yoyote mwenye IQ (Intelligence Quotient) chini ya 70.
Upungufu wa akili ni hali ya kuwa na mapungufu katika ukuaji (development deficit) yanayoanza utotoni ambayo husababisha kupungua uwezo wa kusoma (intellect), kutafakari, utambuzi na kutoweza kuendana na majukumu ya kila siku ya maisha.
Ukubwa wa Tatizo (Epidemiology)
Upungufu wa akili ni tatizo kubwa sana duniani.Huathiri asilimia 1-2 ya watu wote duniani.Huonekana sana kwa wanaume kuliko wanawake (inakisiwa huonekana mara mbili zaidi kwa wanaume kuliko wanawake). Upungufu wa akili wa kati (mild mental retardation) huonekana sana kwa watu wa kipato cha chini lakini upungufu wa akili wa kiwango cha juu hutokea uwiano sawa katika jamii ya matabaka yote na huonekana sana katika umri kati ya miaka 10 hadi 14.
Upungufu wa akili sio ugonjwa (axis II disorder in DSM-IV) kutokana na dalili na viashiria vyake bali ni tatizo la mfumo wa utambuzi wa watu wenye kuhitaji huduma za kijamii na elimu maalum ili kuweza kumudu majukumu yao ya kila siku. Mara nyingi upungufu wa akili hutokea kabla ya mtu kufikisha umri wa miaka 18. Tungependa kwa yoyote mwenye takwimu kutoka afrika mashariki za tatizo hili la upungufu wa akili kutoka katika hospitali za magonjwa ya akili za Butabika National Referral and Teaching Mental Hospital (Kampala, Uganda), Port Reitz District Hospital (Mombasa, Kenya), Mathare Mental Hospital (Nairobi, Kenya), Lutindi Mental Hospital (Tanga, Tanzania) na Mirembe Psychiatric Referral Hospital (Dodoma, Tanzania).
Tabia za Kuendana na Mazingira (Adaptive behavior) ni Nini?
Tabia za kuendana na mazingira ni jinsi mtu anavyoweza kumudu matakwa ya kujihudumia mwenyewe kila siku pasi na kumtegemea mtu yoyote kutokana na umri wake, tabaka lake, utamaduni pamoja na jamii inayomzunguka kutokana na vipengele viwili kati ya hivi vifuatavyo;
- Mawasiliano (Kuweza kuwasiliana na watu)
- Kuweza kujihudumia katika shughuli zinazohitaji kutumia akili (functional academic skills)
- Kuweza kuishi mazingira ya nyumbani na kazini
- Kuwa na uwezo wa kuchanganyikana na jamii katika masuala ya afya na usalama wake
- Kuweza kutumia huduma za jamii ambazo zitamfanya kuishi maisha ya furaha
Ni vizuri kutambua ya kwamba tabia hizi hutegemea sana elimu, uhamasishaji, tabia za mtu binafsi, kupewa fursa za kijamii na za kiufundi (vocational skills), matatizo ya akili na magonjwa mbalimbali ya akili.
Intelligence kitaalamu ni uwezo wa ubongo katika kufikiri, kutatua matatizo, kuchagua au kuwa na busara (reason), na kuelimika.
IQ= Mental age (Umri wa akili) × 100
Chronological age (Umri wa kawaida wa binadamu)
Makundi ya Upungufu wa Akili Kundi Kipimo cha IQ
Upungufu wa akili uliopitiliza kabisa (Profound Mental Retardation) Chini ya 20
Upungufu wa akili mkubwa (Severe Mental Retardation) 20-34
Upungufu wa akili wa kati (Moderate Mental Retardation) 35-49
Upungufu wa akili (Mild Mental Retardation) 50-69
Upungufu wa akili wa kawaida (Borderline Intellectual Functioning) 70-84
Mtu aliye kwenye kundi la upungufu wa akili (Mild Mental Retardation) anaweza kuelimika, na Yule aliye na upungufu wa akili wa kati, mtu huyu anaweza kufunzwa kazi za kumuwezesha kumudu maisha yake ya kila siku. Wale walio na upungufu wa akili mkubwa (Severe MR) na kundi la waliopitiliza (Profound MR) hawawezi kufunzwa chochote na kufundishika.
Kwa hiyo mtoto aliye na umri sawa wa akili na umri sawa wa kibinadamu atakuwa na kipimo cha akili 100 (yaani IQ=100). Kwa wale watoto wenye vipaji maalum, kipimo cha akili yao huwa zaidi ya 100 (IQ>100), na kwa wale wenye akili ya kawaida kipimo cha akili huwa chini ya 100 lakini hakishuki chini ya 85.
Upungufu wa Akili wa Kawaida (Borderline Mental Retardation)
Huwa na akili yakipimo cha IQ= 70-85%. Wanauelewa mdogo shuleni (Slow learners) lakini wanaishi maisha ya kawaida yaani bila kupata taabu yoyote katika maisha yao ya kila siku na wanaweza kuajiriwa.
Upungufu wa akili (Mild Mental Retardation)
Huwa na akili ya kipimo cha IQ=50-70. Asilimia kubwa ya watu wenye upungufu wa akili huwa kwenye kundi hili (asilimia 85-95). Wanatambulika kama wanaoweza kuelimika. Wanaweza kujifunza kusoma, kuandika, na kufanya hesabu rahisi rahisi (simple arithmetic calculations). Hawa wanahitaji shule maalum ili waje kuweza kumudu majukumu yao ya maisha ya kila siku baada ya muda mrefu.Wanakuwa na upungufu mdogo katika uwezo wao wa kuhisi na utambuzi wa vitu (minimal sensorimotor deficits) na ni vigumu kutambua kwamba wanaupungufu wa akili mpaka baadae maishani. Katika ujana wao wanaweza kupata elimu hadi darasa la sita.Ukubwani, hupata uwezo wa kujihudumia wenyewe katika mahitaji yao ya kila siku lakini wanahitaji uangalizi, ushauri, kupewa mwongozo katika majukumu yao ya kifamilia na hasa wanapopata msongo wa mawazo au wakati wamepata matatizo ya kiuchumi.
Upungufu wa Akili wa Kati (Moderate Mental Retardation)
Huwa na akili yakipimo cha IQ=35-50. Asilimia 10 tu ya watu wote wenye upungufu wa akili ndio huwa kwenye kundi hili.Wanatambulika kama wasioweza kufundishika (untrainable) ingawa wengi wao wanaweza kuelimika. Utotoni mwao wanakuwa na mawasiliano mabaya ya kijamii, lakini wanaweza kujifunza kuzungumza, kutambua majina yao na baadhi ya maneno rahisi ambapo kutokana na haya ambayo nimeelezea hapo juu, kwa sasa wanatambulika kama kundi linaloweza kufundishika.Kawaida, huacha shule baada ya kufika darasa la pili (Standard 2). Wanaweza kufundishika katika kazi ambazo hazihitaji kutumia akili ama kazi za mikono.Msongo wa mawazo huathiri mafunzo yao hivyo ni muhimu kuboresha mazingira yao na kuwahudumia vizuri ili wasipate msongo wa mawazo.
Mara nyingi, uwezo wao wa kuelewa watu wanapozungumza ni mzuri kuliko uwezo wao wa kuzungumza na hii huwafanya kupata msongo wa mawazo. Uzungumzaji wao ni wa kawaida na hueleweka vizuri na wale wanaoishi nao au wale wanaofahamiana nao vizuri. Vitendo kama uvaaji nguo, kula, na kujiweka msafi, huchukua muda mrefu kwao kujifunza. Wanahitaji msaada katika matumizi ya hela na hata kuvuka barabara.
Upungufu wa Akili Mkubwa (Severe Mental Retardation)
Huwa na akili ya kipimo cha IQ=20-35 na huonekana kwa watu wenye upungufu wa akili kwa asilimia 5 tu. Hutambulika mapema kwa kutokuwa na uwezo wa kutambua vitu mbalimbali (Poor motor development). Watu hawa hawana uwezo wa kuzungumza na kuwasiliana au hupata uwezo huo baadae maishani. Huitaji shule maalum pamoja na wataalamu wa tiba ya sauti ili waweze kujifunza kuzungumza.Chini ya uangalizi, huweza kujifunza shughuli ndogondogo.
Upungufu wa Akili Uliopitiliza (Profound Mental Retardation)
Huwa na akili ya kipimo cha chini ya 20 yaani IQ<20. Asilimia 1-2 ya watu wenye upungufu wa akili ndio walio kwenye kundi hili. Mara nyingi wanakuwa na ugonjwa au matatizo ya sehemu ya mishipa ya fahamu ambayo husababisha upungufu wa akili.Dalili za kuwa na uwezo finyu wa kutambua na kuhisi mambo mbalimbali, kushindwa kuelimika, kujihudumia, kufanya kazi, kujitunza huonekana mapema sana. Huitaji msaada wa kijamii pamoja na kuhudumiwa katika maisha yao ya kila siku.
Aina za Upungufu wa Akili
Kuna aina mbili za upungufu wa akili ambazo ni;
1.Syndromic mental retardation – Hii ni upungufu wa akili (intellectual deficits) unaoambatana na magonjwa mbalimbali pamoja na viashiria na dalili za kitabia (behavioral signs).
2.Non syndromic mental retardation – Upungufu huu wa akili hausiani na magonjwa au ugonjwa wowote.
Pathofiziologia (Pathophysiology)
Upungufu wa akili ni mjumuiko wa matatizo katika mfumo wa fahamu (CNS functions) ambapo sehemu inayojulikana kama cortical structures (ambayo huusisha pamoja na sehemu zingine kama hippocampus na medial temporal cortex) ndio huathirika. Watu wengi wenye upungufu wa akili hawaonyeshi kuathirika katika mfumo wao wa fahamu. Ni aslimia 10-15 ya watu wote wenye upungufu wa akili ambao ndio wanaonyesha kuathirika katika mfumo wao wa fahamu.
Matatizo katika mfumo wa fahamu ambayo huonekana sana ni kichwa maji (hydrocephalus), neural tube defects, microcephaly na (disorders of migration- the lissencephalis na muunganiko wa mwatuko wa ubongo {agenesis of corpus carlosum} ambayo huonekana mara chache).
Watu wengi wenye upungufu wa akili aina ya mild mental retardation na wenye matatizo mengine ya ufahamu (other learning disorders), huwa hawana matatizo katika mfumo wao wa fahamu, madhara katika neva na dysmorphisms lakini wanauwezekano mkubwa wa kutoka katika familia zenye hali duni ya kiuchumi, familia yenye kipimo cha akili ndogo (low IQ), na elimu duni.
Nini husababisha upungufu wa akili?
Zipo sababu nyingi ambazo husababisha upungufu wa akili ambazo ni kama ifuatavyo;
- Matatizo ya kurithi (genetic factors)
- Antenatal factors
- Postnatal factors
- Matatizo ya kijamii na kitamaduni (socio-cultural factors)
Magonjwa ya akili (psychiatry disorders)
Thuluthi moja (1/3) ya watu wenye upungufu wa akili chanzo hasa hakijulikani.
Matatizo ya viashiria vya urithi (genetic factors)
- Chromosal abnormalities kama down syndrome, fragile X syndrome (mgonjwa anakuwa na kichwa kikubwa, masikio makubwa kama ya popo, uso mrefu, korodani kubwa kupitiliza na nyayo zinakuwa bapa {flat feet},huwa na matatizo ya lugha na sauti, hii husababishwa na matatizo katika ncha ya mkono mrefu wa chromosome)
- Metabolic disorders kama phenylketonuria, homocystinuri, galactosemia nk.
- Magonjwa kwenye ubongo (Gross disease of the brain) kama cerebral dysgenesis, tuberose sclerosis, neurofibrosis nk.
Madhara ya kwenye ubongo (brain malformations) kama nueral tube defects, kichwa maji na microcephalus
Antenatal factors
- Matatizo ambayo hutokea wakati mtoto bado hajazaliwa (yaani yanayompata mtoto wakati bado yupo tumboni mwa mama yake). Haya yanaweza kuwa;
- Magonjwa kama ugonjwa wa kaswende (syphilis), TORCH
- Sumu (intoxications) kama madini ya risasi (lead), madawa ya kulevya, unywaji pombe wakati wa ujauzito nk.
- Physical damage – Tiba ya mionzi au vipimo vya mionzi, injury, ukosefu wa hewa ya oksijeni kwa mtoto (hypoxia).
- Matatizo ya kondo la uzazi (Placental dysfunctions) – Toxaemia, ukosefu wa virutubisho sahihi katika ukuaji wa kondo (Nutritional growth retardation).
- Matatizo katika mfumo wa vichocheo mwilini (Endocrine disorders) – Hypothyroidism (ugonjwa wa tezi la koo), ugonjwa wa kisukari kwa mama mjazito, hypoparathyroidism.
Perinatal factors
- Matatizo yanayotokea wakati mtoto anazaliwa (wakati wa kujifungua kwa mama mjazito)
- Ukosefu wa hewa ya oksijeni (Birth asphyxia), cerebral palsy nk
- Madhara ya mtoto kuzaliwa njiti (complications of prematurity) kama uvujaji damu ndani ya ubongo (intraventricular haemorrhage).
- Hypoxic Ischemic encephalopathy
Post-natal factors
- Matatizo yanayotokea baada ya mtoto kuzaliwa
- Injury – Head injury (kuumia kichwa)
- Sumu (Intoxication) kutokana na madini ya risasi, mercury nk.
Magonjwa kama ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis), encephalitis (maambukizi kwenye ubongo)
Socio-cultural factors (Matatizo ya kijamii na kitamaduni)
Kutokuwa na uwezo wa kujumuika na jamii huchochewa na ukosefu wa elimu, kiwango duni cha uhamasishaji, tabia ya mtu, ucheshi wa mtu,utapia mlo, mimba za utotoni (kwani huleta umaskini, utapia mlo, afya duni, kuathirika kwa mama na hivyo kumuathiri mtoto), vocational opportunities pamoja na magonjwa ya akili na magonjwa mbalimbali.
Kukosekana kwa vichocheo hivyo au kuwepo kwa magonjwa ya akili na baadhi ya magonjwa mbalimbali huweza kusababisha upungufu wa akili. Ikumbukwe ya kwamba akili ya mtoto huwa inakuwa kwa hiyo ni muhimu apewe fursa ya kuweza kukuza akili yake.
Magonjwa ya akili (Psychiatric disorders)
- Pervasive developmental disorders (Autistic spectrum disorders).
Image Source: https://newrepublic.com
Baadhi ya watu hukumbwa na tatizo la kuwa na vijiwe katika figo na mfumo wa mkojo kwa ujumla. Mawe haya hutokana na ama madini chumvi au tindikali mbalimbali zinazotolewa mwilini.
Aina za mawe katika figo
Aina za vijiwe katika figo ni pamoja na
- vijiwe vya calcium oxalate
- vijiwe vya tindikali ya uric (uric acid)
- Vijiwe vya struvite (magnesium, ammonium na phosphate)
Vijiwe katika figo husababishwa na nini?
Kwa kiasi kikubwa, vijiwe husababishwa na kukosekana kwa usawa wa maji, madini na tindikali mwilini yaani electrolyte imbalance.
Dalili na Viashiria vya Upungufu wa Akili
- Kuchelewa katika ukuaji wa uwezo wa kuongea/kuzungumza
- Upungufu wa kumbukumbu (deficits in memory skills)
- Matatizo katika kufahamu mambo ya kijamii
- Upungufu wa uwezo wa kutatua matatizo
- Kuchelewa kukua kwa tabia za vitendo vya kujihudumia mwenyewe (kama kufunga vifungo vya shati nk)
- Kuendelea kuwa na akili za kitoto
- Kupungua uwezo wa kusoma