Karibuni tena katika kijiwe chetu,leo kwenye muendelezo wa makala zetu kuhusu udhibiti wa kisukari tunaangalia umuhimu wa tendo la ndoa katika kusaidia kupunguza kiwango cha juu ya sukari.
Kwa upande moja ama mwingine tendo la ndoa ni moja ya zoezi la mwili kama mazoezi mengine kama kukimbia na mazoezi mengine ya viungo na pia tendo hili linasaidia sana kushuka kiwango cha sukari, Moja ya tafiti iliyowahi kufanya na American Journal of Medicine inasema kuwa mtu akifanya tendo la ndoa mara tatu au nne kwa wiki anajiweka kwenye nafasi ya kutopata matatizo ya msongo wa mawazo ambayo unaweza kuleta matatizo kama ya Kisukari na Presha.
Moja ya tafiti iliyofanywa na Taasisi ya Kisukari Marekani (ADA) zinaonesha kuwa kufanya tendo la ndoa husaidia kuyeyusha mafuta na sukari mwilini kwakuwa ni moja ya mazoezi ya viungo.Tafiti zingine zinaonesha kuwa endapo mtu ukifanya tendo la ndoa mara tatu au nne kwa siku husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini.
KWA kawaida mwanaume ana korodani mbili ambazo zimehifadhiwa katika mfuko maalum wenye tabaka tatu na ndani kuna kiasi kidogo cha maji kinachozunguka korodani ili kuilinda. Mwanaume endapo atakuwa na korodani moja ni tatizo na pia akiwa hana kabisa korodani ni tatizo kubwa.
Kazi ya korodani ni kuzalisha mbegu za kiume, mwanaume anaweza kuwa na korodani zote mbili lakini akashindwa kuzalisha mbegu za uzazi kutokana na matatizo mbalimbali.
Mwanaume mwenye korodani moja anaweza kuzalisha mbegu au asizalishe kabisa, kitu cha msingi akapimwe hospitali kuona uwezo wa hiyo moja. Mwanaume ambaye hana korodani kabisa hawezi kuzalisha mbegu za uzazi hivyo hana uwezo wa kumpa mimba mwanamke. Tatizo la kuwa na korodani moja au kukosa kabisa tutakuja kuliona katika makala zijazo.
JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA
Maumivu ya korodani hutokea katika korodani au haswa moja au zote mbili endapo zitaumizwa kwa kuumia au maambukizi. Maambukizi haya yanaweza kuwa makali na ya muda mfupi,yanakuwa makali kwa muda fulani halafu yanapoa yenyewe au kwa dawa baadaye yanarudi tena yakiwa makali sana kama mwanzo au pia huwa sugu yaani unakuwa na maumivu ambayo siyo makali ila ni ya muda mrefu na yanayokunyima raha.
Maumivu ya korodani yanaweza kuwa makali kiasi kwamba yatahitajika matibabu ya dharura mfano korodani inavimba kama jipu kubwa, ikiambatana na maumivu makali na homa, tatizo hili kitaalam huitwa ‘Fournier's gangrene' au inatamkwa ‘Fonias gangrini'.
Vilevile inaweza kutokea korodani ikajinyonga yenyewe na kusababisha ukapata maumivu makali ya ghafla yanayoelekea hadi tumboni, tatizo hili linaitwa Testicular Torsion. Matatizo haya kwa ujumla wake tutakuja kuyaona katika makala zijazo.
CHANZO CHA TATIZO
Maumivu ya korodani yana vyanzo mbalimbali, lakini maumivu sugu ni yale yanayochukua takriban zaidi ya miezi mitatu. Maumivu makali na ya ghafla huwa hayavumiliki na huwa na tiba ya dharura. Maumivu haya sugu huwa kwa kipindi fulani hasa kwa wanaume ambao wametoka kufunga uzazi Vesectomy lakini baadaye hupoa. Vilevile husababishwa na maambukizi katika korodani na kusababisha magonjwa kama Epididymits, Prostatis na Orchitis ambayo yote ni maradhi ya viungo vya uzazi vya mwanaume na husababisha ugumba.

Baadhi ya watu wana meno yaliyojipanga visivyo. Katika hali ya kawaida meno yanatakiwa yawe katika mahusiano mazuri kiasi kwamba meno ya juu yaweze kukutana vizuri na yaliyo jirani yakae vizuri pia. Utakuta baadhi ya watu meno ya juu yamechomoza mbele sana kiasi kwamba hata kufunga mdomo ni tatizo, wengine ya chini kuvutika mbele zaidi na kuwa na kidevu kilichochongoka kwenda mbele na wengine yamepandana pandana.
Mpangilio mbaya wa meno unaweza kuwa mbaya zaidi kiasi cha kumughasi mhusika na wakati mwingine meno yenyewe kushindwa kufanya kazi zake vizuri. Tatizo lingine la meno yaliyojipanga vibaya ni vigumu kuyasafisha na hivyo kuyaweka meno katika hatari ya kuoza na kusababisha magonjwa ya fizi.
Nini kinasababisha matatizo haya?
- Maumbile yatokanayo na vinasaba na urithi
- Tabia kama kunyonya vidole utotoni hata ukubwani kwa wengine
- Kuwahi kutoka meno ya utotoni
- Kuchelewa kutoka kwa meno ya utotoni hivyo kuyafanya ya ukubwani kuota upande
- Ajali wakati wa kujifungua ambayo inaweza kuathiri maeneo ya kukua kwa taya
Matibabu
Lengo kubwa la matibabu ni kuyaweka meno katika mpangilio unaokubalika, ili kuboresha muonekano, utafunaji na hata utamkaji wa maneno.
Katika sehemu ya kwanza ya makala hii ya maambukizi ya fangasi, tuliangalia aina za fangasi, watu waliopo kwenye hatari ya kupata maambukizi ya fangasi na aina ya maambukizi ya fangasi. Katika sehemu hii ya pili na ya mwisho katika muendelezo wa makala hii, tutaangalia maambukizi ya fangasi kwenye damu yaani systemic mycoses.
Systemic Mycoses
Ni maambukizi ya fangasi kwenye damu ambayo huanzia kwa fangasi kuvamia mapafu ya mtu.Maambukizi haya yamegawanyika katika sehemu kuu mbili;
- Maambukizi ya fangasi kutokana na fangasi wa kawaida kwa watu wenye afya njema (Systemic mycoses due to primary pathogens)
- Maambukizi ya fangasi kwenye damu kutokana na fangasi nyemelezi kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini (Systemic mycoses due to opportunistic pathogens)
Maambukizi ya fangasi kutokana na fangasi wa kawaida kwa watu wenye afya njema (Systemic mycoses due to primary pathogens)
Maambukizi haya ya fangasi huanzia kwenye mapafu na kusambaa kwenye viungo vingine vya mwili.Yafuatayo ni maambukizi ya fangasi kwenye damu yanayoonekana sana kwa wagonjwa nayo ni;
- Histoplasmosis
- Blastomycosis
- Coccidioidomycosis
Histoplasmosis
Husababishwa na fangasi Histoplasma Capsulatum, ambao huishi kwenye mazingira hasa kwenye mchanga na mtu huweza kupata maambukizi ya fangasi hawa kwa kuvuta hewa yenye mazalia ya fangasi (Fungal spores).Watu wenye maambukizi haya huweza kuambukiza watu wengine au hata kuambukiza wanyama. Maambukizi ya histoplasmosis ni hatari sana kwa watu wenye kinga dhaifu mwilini hasa kama yatasambaa kwenye viungo vingine vya mwili.
Dalili na Viashiria ya maambukizi ya Histoplasmosis
- Homa kali
- Uchovu
- Kutetemeka (Chills)
- Maumivu ya kichwa
- Maumivu ya kifua
- Maumivu ya mwili (Body aches)
Vipimo vya uchunguzi
- Uchunguzi wa maabara kwa kutumia hadubini
- Kuotesha fangasi maabara
- Ugunduzi wa surface markers za fangasi aina ya Histoplasma Capsulatum kwenye mkojo
- Vipimo vya damu vya kuangalia jinsi kinga za mwili zinavyojitahidi kukabiliana na maambukizi haya (Antibody response to histoplasma)
Tiba ya Histoplasmosis
- Mara nyingi maambukizi haya hupona yenyewe kwa wale wanaopata maambukizi ya wastani
- Kwa wale wenye kupata maambukizi hatari, uhitaji matibabu ya dawa za kutibu fangasi
Blastomycosis
Husababishwa na fangasi aina ya Blastomyces dermatitidis.Maambukizi haya huathiri mbwa, binadamu, simba, farasi nk. Blastomycosis huweza kuenezwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine au kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu.
Dalili na Vishiria vya Blastomycosis
- Homa kali inayoambatana na mtetemo (Chills)
- Maumivu ya kifua
- Kukohoa
- Kushindwa kupumua vizuri
- Maumivu ya misuli (Muscle aches)
- Maumivu ya viunganishi vya mifupa (Joint pain)
Vipimo vya Uchunguzi
- Kuoteshwa kwa fangasi maabara (Culture)
- Kuchunguza tishu maabara kwa kutumia hadubini
- Kipimo cha antigen test - Kinaweza kugundua uwepo wa fangasi kwa kupima mkojo au damu (Serum)
Tiba ya Blastomycosis
- Dawa za kutibu fangasi – Hutumika kwa muda mrefu
Madawa ya kulevya yameleta athari sana katika jamii, kutokana na ile hali ya kufanya hisia ya utegemezi, kwamba mtu anaona hawezi kufanya chochote bila kupata japo kidogo.
Kuna aina nyingi za madawa ya kulevya ila aina mbili ndio ambayo yanasumbua sana,
- Cocaine
- Heroin
Cocaine hutokana na majani ya mmea uitwao kitaalamu Erythroxylon coca, na huandaliwa kwa kupitia hatua mbali mbali na hatua moja wapo ni ya kupata kinachotumika kuengenezea soda za cola, na hatua ya mbele zaidi ndio cocaine. matumizi yake ni kwa kujichoma sindano, na wengine huvuta aidha kwa kuunguza kwanza ambao huitwa‘crack’ , mpaka mwaka 2007,Marekani ilikuwa na watumiaji million 2.1, na kati ya hao million 1.6 walikuwa tegemezi au mateja , na matumizi ya kawaida au ya kupitiliza ya cocaine yalipekea asilimia 30% kuhudhuria hospitali kutokana na athari zake, na wengi hufika hospitali wakilalamika maamumivu makali ya kifua.
.
Kutoka katika jarida la Circulation Vol.122, issue24 liliotolewa Desemba 2010, waliripoti kati ya wagonjwa 233 ambao ni watumiaji wa cocaine katika idara ya dharura asilimia 56% walikuwa na athari kwenye moyo na asilimia 40% walilalamika kuwa na maumivu ya kifua. Taarifa za hvivi karibuni inaonyesha marekani ina watu milion 30 ambayo wametumia cocaine na milioni 5-6 ni tegemezi au mateja (taarifa kutoka jarida la national medical association)
Heroin hutoka kwenye ua kitaalamu hujulikana papaver somniferum- opium poppy, katika karne ya 18, madaktari walitumia kama dawa ya kupunguza maumivu hasa kwa wagonjwa wa saratani, pepopunda, hedhi. Mwishoni mwa karne ya 18 ndio madaktari waligundua hali ya tegemezi ya kulevya iliyoletwa na heroin. Huandaliwa kupitia hatua mbali mbali na hatua moja wapo ni dawa ambayo hutumiwa kupunguza maumivu kitaalamu Morphine, na hatua za mbele zaidi ndio heroin. Heroin hutumika kwa njia ya kunusa na kuvuta puani na kujichoma sindano
Cocaine na Heroin zote hulevya kukupa hali ya kujisikia furaha kitaalamu Euphoria, ila hupelekea kuwa tegemezi wa kulevya huko.
Habari! Karibuni tena katika muendelezo wa makala zetu kuhusu Kisukari ambazo zinapatika katika tovuti pendwa ya TANZMED, Mara ya mwisho tulikumbushana kuwa wewe ndio tabibu ama daktari wa tatizo lako, wewe sio mgonjwa wewe ni mtu wenye kisukari, ama una ishi na kisukari, ni kitu cha kawaida sana kwa dunia ya sasa.
Sasa leo napenda kuwakumbusha ni vitu gani au ni mambo gani mtu wenye kisukari anatakiwa kuviepuka. Kama tujuavyo kuwa endapo Kisukari haitadhibitiwa ipasavyo basi inaweza kuleta madhara mengi kama kupata kiarusi,upofu, matatizo ya moyo, vidonda ndugu,matatizo ya figo na ini,kwa wanaume kukosa nguvu vya kiume, matatizo ya misuli na kadhalika. Sasa kwa sisi wenye kisukari tuishi vipi ama tufanye nini ili kuepuka haya yote?
- Jambo la kwanza ambalo mara nyingi napenda kuwakumbusha watu watu wenye kisukari kuwa ni muhimu sana kujikubali, hili ni jambo ya kwanza kwakuwa ukijikubali kuwa una tatizo la kisukari inakuwa rahisi sana kubadili mfumo wa maisha uliyokuwa unaishi kabla ya kupata tatizo na mara nyingi nasisitiza umuhimu wa kumpatia ushauri nasaha kwa watu wenye kisukari.
- Jambo la pili ni kuepuka kabisa na kupunguza kutumia vitu ama vyakula vinavyoweza kupandisha sukari yako kwa haraka,vitu kama soda,juisi,keki,sukari,asali, Chokoleti na vitu vya kupunguza hasa hasa ni vyakula vya wanga na matunda,hapa nikisema matunda simaanishi kuwa matunda walisiwe hapana,ninachomaanisha hapa ni liliwe tunda na sio matunda na kwa muda, ima masaa mawili au lisaa limoja baada ya chakula.
- Jambo la tatu ni kuepuka kupata vidonda kwa kuwa kama hujaweza kudhibiti kisukari ni rahisi sana kidonda kuchelewa kupona kwa hiyo basi yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ya kuizngatia;
- Epuka kutembea bila viatu,yaani kutembea peku, kwa maana unaweza kujikata na kitu chenye ncha kali kama sindano, chumba, miiba nk
- Epuka kutumia vitu vyenye ncha kali kutaka kucha kwa mfano usitumia wembe au mkasi kukata kucha ili kuepuka kupataka na kupata kidonda,pendelea sana kutumia nail taker.
- Epuka kuvaa viatu na soksi za kubana, na pia hakikisha miguu yako ni mikavu kila muda, kwa hiyo basi utokapo kuoga ama kunawa miguu, hakikisha unaikausha vizuri hasa katikati ya vidole, kwa sababu kama ukiacha unyevunyevu ni rahisi kutengeneza lengelenge na pia endapo utapata lengelenge usitumbue, acha na likaule lenyewe
- Kwa wanawake, epuka kuvaa viatu virefu kwa sababu vinazuia damu kufanya mvunguko wake wa kawaida (blood circulation)
Kwa kumalizia napenda kusisitiza tu kuwa kisukari sio mwisho wa maisha,na pia kumbuka kuwa watu wenye kisukari ni watu wanaoishi katika mfumo sahihi wa maisha.
Saratani ni aina ya ugonjwa unaosababisha ukuaji wa seli za mwili kubadilika na kukua bila mpangilio maalum.
Saratani ya matiti hutokea kwenye titi ambalo kwa kawaida lina sehemu ya kutengeneza maziwa ijulikanayo kama lobules na aina fulani ya mishipa inayounganisha hizi lobules na chuchu za titi. Sehemu kubwa iliyobakia ya matiti inajumuisha mafuta na tishu ambazo kitaalamu tunazoita connective and lymphatic tissue. Saratani ya matiti inayotokea kwenye lobules huitwa lobular carcinoma na ile inayotokea kwenye ducts huitwa ductal carcinoma.
Baadhi ya saratani ya matiti zinaongeza ukubwa kutokana na kuwa na vishikizi aina ya receptors zinazojulikana kama estrogen receptors kwenye seli zao ambazo husababisha ukuaji wa saratani ya matiti.
Kuna wanawake wengine wana viashiria vya asili vinajulikana kama HER2 positive breast cancer ambacho husaidia seli kuongezeka, kugawanyika na kujirekebisha pale zinapoharibika. Kiashiria hiki kinaaminika ndicho kinachosababisha wanawake hawa kuwa na saratani ya matiti yenye madhara zaidi na kuwa na uwezekano mkubwa wa kujirudia kwa saratani baada ya tiba tofauti na wale ambao hawana kiashiria hiki cha HRE2.
Vihatarishi vya Saratani
Kuna mambo kadhaa ambayo yameonekana kuwa na uhusiano, ama wa moja kwa moja au kwa kupitia vitu vingine, wa kusababisha saratani ya matiti, au kumfanya mtu au kundi la watu kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa huu kuliko wengine. Mambo hayo ni pamoja na
Ugonjwa wa kichocho, ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vinavyojulikana kwa kitaalamu kama schistosoma. Ugonjwa huu huathiri zaidi ya watu milioni 207 duniani na kati ya hao asilimia 85% ni katika bara la Afrika. Baada ya ugonjwa wa malaria na maambukizi ya minyoo, kichocho ni wa tatu katika magonjwa makubwa ya kitropiki.
Kichocho ni ugonjwa ambao huathiri eneo fulani la jamii au eneo fulani la kijiografia kwa kitaalamu tunaita endemic, ambapo watu wanaathirika kutokana na shughuli zao za kila siku mfano wakulima, wavuvi, na vilevile kutokana na starehe kama kuogelea kwenye bwawa lisilo salama au ziwani.
Kichocho huambukizwaje?
Maambukizi ya ugonjwa huu wa kichocho hutokea pale mabuu (larvae) ya vimelea vya shistosoma yalioachiwa kutoka kwa konokono wa majini yanapopenya ngozi ya mtu aliye kwenye maji yalioathiriwa.
Ndani ya mwili wa binadamu haya mabuu (larvae) huendelea kukomaa na kuwa vimelea kamili, vimelea hivi hupenda kuishi kwenye mishipa ya damu, vimelea jike hutaga mayai, ambapo baadhi ya mayai hutolewa kwa kukojoa au kwa njia ya haja kubwa. Na mzunguko huendelea.
Kuna aina ngapi za kichocho?
Kuna aina mbili za kichocho ambazo ni:
- Kichocho cha utumbo ama intestinal schistosomiasis na
- Kichocho cha mfumo wa mkojo ama urinary schistosomiaisis
Kila aina ya kichocho kinaletwa na aina tofauti za vimelea hawa wa schistosoma kama ifuatavyo:
- Kichocho cha Utumbo (Intestinal schistosomiasis) husababishwa na vimelea vya Schistosoma mansoni na Schistosoma intercalatum
- Kichocho cha Utumbo aina ya Asia (asian intestinal schistosomiasis) husababishwa na vimelea aina ya Schistosoma japonicum na Schistosoma mekongi
- Kichocho cha mkojo (Urinary schistosomiasis) husababishwa na vimelea jamii ya Schistosoma hematobium
Dalili za kichocho
- Maumivu ya tumbo
- Kuhara damu hasa kwa kichocho cha utumbo
- Kukojoa damu (terminal hematuria) hasa kwa kichocho cha mkojo
- Kikohozi
- Homa
- Uchovu
- Ngozi kuwasha (cercarial dermatitis) kwa jina lingine swimmers itch
Vipimo na Uchunguzi
- Kuangalia uwepo wa mayai ya vimelea kwenye mkojo na kinyesi kwa kutumia Hadubini.
- X-ray ya tumbo
- Ultrasound ya tumbo
- Kipimo cha damu (complete blood count)
- Cystoscopy kwa kichocho cha mkojo
- Sigmoidoscopy/proctoscopy kwa kichocho cha utumbo
Matibabu
- Kichocho hutibiwa kwa kutumia dozi ya mara moja ya dawa iitwayo Praziquantel
Madhara ya Kichocho
- Kansa ya kibofu cha mkojo (cancer of urinary bladder)
- Figo kushindwa kufanya kazi
- Cor pulmonale
- Gastrointestinal bleeding - Kuvuja damu ndani ya mwili hasa katika mfumo mzima wa chakula
- Portal hypertension
- Seizures - Kifafa au degedege
- Reflex nephropathy
Jinsi ya kuzuia kichocho
- Kuondoa na kuangamiza konokono waliopo kwenye maji au ambao hupenda kuishi kwenye maji ambao ni muhimu katika mzunguko wa kuuwaji wa vimelea vinavyoleta kichocho kwa kutumia Acrolein, copper sulfate na niclosamide.
- Kwa sasa kuna utafiti unaendelea kwa ajili ya kutafuta chanjo ya ugonjwa huu wa kichocho.
Watu wengi huwa na hofu ya sintofahamu hasa wanapofikiria kwenda kumwona daktari wa meno. Mambo 10 yafuatayo yatakusaidia sana kufahamu nini utarajie unapokwenda kufuata uchunguzi wa afya ya kinywa na meno ama matibabu ya magonjwa ya kinywa na meno.
1. Uchunguzi wa afya ya kinywa na meno hujuimuisha uchunguzi wa kansa kinywani
Unapokwenda kwa daktari wa kinywa na meno kwa uchunguzi wa kawaida wa kinywa na meno (dental check up visit), kwa kawaida daktari wa kinywa na meno hutazama hali ya kinywa na meno pia huchunguza uwepo wa dalili za kansa kinywani. Inakadiriwa kuwa mtu mmoja hufa kila saa la kutokana na ugonjwa wa kansa kinywani huko Marekani. Ugonjwa huu hatari unaoshambulia zaidi kuta za kinywa, midomo-hasa mdomo wa chini- pamoja na koo unatibika ikiwa utatambuliwa mapema na kutibiwa kikamilifu.
Hivyo, kumwona daktari wa meno walau mara mbili kwa mwaka (kila baada ya miezi sita) na kuepuka matumizi ya tumbaku/sigara vitakuwezesha kujikinga na ugonjwa wa kansa ya kinywa na madhara yake.
2. Magonjwa ya fizi huathiri afya ya mwili kwa ujumla
Magonjwa ya fizi na meno ni chanzo kikuu cha kupoteza meno kwa watu wenye umri mkubwa/watu wazima, na pia magonjwa haya huhusishwa na magonjwa ya moyo na kiharusi (stroke).
Ikiwa magonjwa haya ya fizi yatatambuliwa mapema (gingivitis), yanatibika vizuri na kuepusha madhara zaidi.
Ikiwa tatizo hili halitopata tiba mapema, ugonjwa hukomaa zaidi (periodontitis) ambapo mfupa unaoshikilia jino/meno hushambuliwa na kuharibiwa.
Kusafisha meno kwa kupiga mswaki mara mbili kwa siku, matumizi ya nyuzi-safishi (dental floss), kumwona daktari wa meno kwa uchunguzi mara kwa mara na kusafisha meno kitaalamu kwa tatibu wa meno, kutasaidia kuepuka madhara ya magonjwa ya fizi.
3. Uchunguzi wa kinywa na kusafisha meno kitaalamu ni tiba muhimu zaidi
Ni wangapi kati yetu wenye desturi ya kumwona daktari wa meno walau mara mbili kwa mwaka (walau kila baada ya miezi sita)? Mara nyingi wengi wetu huhangaika na foleni za kumwona daktari wa meno pale tu tunaposumbuliwa na maumivu ama ya jino ama kidonda kinywani ama kwa sababi ya hali zinginezo zinatotulazimisha kumwona daktari wa meno.
Kusubiri mpaka tusukumwe na maumivu ya meno/kidonda kinywani ama ajali yoyote kunatunyima fursa bora zaidi ya kuchunguzwa afya ya kinywa na meno na kusafishwa meno ili kuepusha madhara ya magonjwa ya kinywa na meno kabla hayajatokea ama kukomaa.
Pingamizi la upumuaji usingizini ni hali ya kushindwa kupumua kwa kutumia pua au mdomo kwa muda wa sekunde 10 wakati mtu akiwa amelala. Tatizo hili hutokea zaidi ya mara 30 katika hatua mbili za vipindi vya usingizi vinavyojulikana kitaalamu kama Rapid Eye Movement na Non Rapid Eye Movement.
Rapid Eye Movement Sleep ni kipindi kimojawapo cha usingizi wa kawaida ambacho huambatana na macho kucheza cheza yaani mtu anakuwa yupo usingizini huku macho yake yakicheza cheza. Kwa kawaida wakati mtu amelala hupitia hatua hii mojawapo ya usingizi na hutokea mara 4-5 katika usingizi, mwanzoni REM ikitokea kwa muda mfupi sana na mwishowe kipindi hiki kukawia kwa muda mrefu hasa inapokaribia asubuhi. Inakisiwa REM huchukua asilimia 20-25 ya usingizi wa mtu mzima yaani dakika 90-120 kwa ujumla.
Non Rapid Eye Movement Sleep ni hatua ambayo mtu anakuwa amelala lakini hapitii hatua ya REM, hivyo kumfanya kutochezesha macho, kuota ndoto ni nadra sana kwa wenye kupata hatua hii, akili huwa katika hali njema kabisa (mindset is more organized) viungo vya mwili wake kutolegea (muscles not paralyzed) ndio maana mtu anaweza kutembea huku akiwa usingizini (sleep walk).